|
Article on other languages:
|
Morisi inaitwa rasmi Jamhuri ya Morisi (Kiingereza: Republic of Mauritius, Kifaransa: République de Maurice) ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi takriban 900 km mashariki ya Madagaska na 4000 km kusini-magharibi ya Bara Hindi. Eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Morisi yenyewe, kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidgo vya Cargados Carajos na Agalega. Hivi vyote ni sehemu ya funguvisiwa ya Maskarena pamoja na kisiwa cha kifaransa cha Réunion. Mji mkuu wa jamhuri ni Port Louis. Eneo la Jamhuri ya MorisiVisiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana: Kisiwa kikuu cha Morisi ni 1,865km² au 91 % za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wote wa wakazi milioni 1.2 huishi hapo. Kisiwa cha Rodrigues kipo 560 km mashariki ya Morisi yenyewe. Eneo lake ni 109 km² kuna wakazi 40,000. Visiwa vya Cargados Carajos (vianitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana vyenye eneo la 1.3 km² pekee. Viko 300 km kaskazini ya Morosi. Kuna wakazi wachache wavuvi Agalega ni visiwa viwili yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini takriban 1,122 Km kaskazini ya Morisi yenyewe. Visiwa vina eneo la 70 km². Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa ha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga wa matumizi wao wenyewe. WakaziWatu wa Morisi ni mchanganyiko kutokana na historia ya visiwa hivi. Wakazi wa kwanza walikuwa Waholanzi hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliacha visiwa na kuondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi. Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi Wafaransa walipeka pia watumwa kutoka Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000 pia Wahindi 587. Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja ya Kifaransa. Baada ya kuwapatia watumwa uhuru Waingereza walileta Wahindi wengi baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi. Lakini 80% ya wananchi hutumia aina ya Kifaransa kama lugha ya kwanza. Asilimia 15 hutumia lugha za Kihindi, wengine Kichina na Kiingereza. Karibu nusu ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 35% Ukristo (hasa Wakatoliki), 12% ni Waislamu Wasunni, 3% Washia, 1% Wabuddha. UchumiHadi leo kilimo cha miwa (sukari) ni mgongo wa uti wa uchumi wa Morisi. Nchi iliendelea na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa na hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni juu kuliko nchi nyingi za Afrika.
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.