|
Article in other languages: |
Aina za serikali duniani
aina za Jamhuri: buluu, kijani, njano na machungwa; Ufalme: nyekundu Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka madogo tu ya kisiasa dhambarau:Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka makubwa dhambarau nyeusi: mfalme ana madaraka yote habanwi na katiba Mengine: Utawala wa chama kimoja au kamati ya kijeshi Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi. Utawala wa kifalme ilikuwa hali ya kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu. Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia". Kama cheo kinaendelea katika ukoo mmoja kutoka mababa kwa watoto wao familia hii huitwa nasaba. Madaraka ya mfalmeMadaraka ya wafalme walitofautiana kati ya nchi na nchi na kati ya kipindi na kipindi cha historia. Mifano ni:
Wafalme wa nchi kama Moroko na Yordani wana athira kubwa zaidi.
Wafalme na watawala wengineHakuna utaratibu sanifu mtawala gani anastahili kuitwa "mfalme". Kwa kawaida anasimamia eneo au nchi ya kujitegemea lakini wengine huweka pia mashariti kuhusu ukubwa wa eneo lake. Kwa maeneo fulani kuna vipindi katika historia ambako si rahisi kutofautisha kati ya wafalme na watawala wadogo wengine kama watemi, machifu n.k.. Mara nyingi watawala wa Waswahili ambao hawakuwa na mamalaka nje ya eneo dogo la mji wao walijiita Sultani na Wareno waliwaita "reyes" (wafalme). Hali hii ililingana na mifano mingine kama kati ya Wagiriki wa Kale ambako vilevile watawala wadogo juu ya miji walitumia cheo cha "mfalme".
Questions for article: |
This article is from Wikipedia. All text is available under the terms of the GNU Free Documentation License.
IHS Europe: Infrared Heating Systems for Home and Business.